UM katika hatua za mwisho za kununua ndege zisizo na rubani zitakazotumika DRC

2 Agosti 2013

Idara ya operesheni za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa imethibitisha kuwa imefikia hatua ya mwisho katika harakati za kuagiza ndege zinazoruka bila rubani kwa ajili ya kujaribiwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO katika ulinzi wa raia. Taarifa zaidi na Joseph Msami. (TAARIFA YA JOSEPH MSAMI)

Ndege hizo zijulikanazo kama FALCO, zimeundwa kuwa na uwezo wa kuruka masafa ya wastani angani, na uwezo wa kubeba vidude vya aina mbali mbali vyenye uwezo wa kurekodi kinachoendelea katika maeneo wanakopaswa kulindwa raia.

Ndege hizo hazina silaha, na zinatarajiwa kupelekwa DRC katika wiki chache zijazo, ili kusaidia katika ulinzi wa raia dhidi ya makundi yenye silaha.

 Ndege hizo zimeagizwa kutoka kwa kampuni moja ya Kiitalia, SELEX ES.Luteni Jenerali Paul Ignace Mella ni kamanda wa kikosi cha kulinda amani Darfur, UNAMID, na wakati wa mkutano wa makamanda wa vikosi vya kulinda amani hapa mjini New York, alitupa maelezo zaidi kuhusu ndege hizo.

 (SAUTI YA LT. JEN. PAUL IGNACE MELLA)