Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yakaribisha kutangazwa Baraza la Mawaziri Sudan Kusini

UNMISS yakaribisha kutangazwa Baraza la Mawaziri Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS umekaribisha hatua ya kuteuliwa kwa baraza jipya la mawaziri nchini humo, ambalo limetangazwa hapo jana Julai 31. Joshua Mmali ana maelezo zaidi(TAARIFA YA JOSHUA)

Kutangazwa kwa baraza jipya, ambalo ni dogo zaidi na lenye muundo ulorekebishwa, kunatoa nafasi mpya kwa serikali kutekeleza majukumu ya kipaumbele kwa ajili ya taifa la Sudan Kusini, imesema UNMISS.

Taarifa ilotolewa leo na UNMISS imesema, ujumbe huo u tayari kushirikiana na baraza hilo jipya mara tu litakapoapishwa, katika kuendeleza ajenda ya mabadiliko Sudan Kusini, ikiwemo kupiga vita ufisadi, kuboresha sekta ya usalama na kutoa huduma muhimu kwa watu wake.

UNMISS imeongeza kuwa inatizamia kushirikiana na baraza hilo katika kuwalinda raia, kuimarisha taasisi muhimu za kitaifa na hatua zilizopigwa kisiasa katika kufanyia marekebisho katiba, pamoja na kuandaa uchaguzi huru na wa haki. Imetoa wito kwa mawaziri hao wapya kudumisha umoja wa kitaifa na heshima ya haki za binadamu kwa raia wote wa Sudan Kusini.