Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saa 48 kwa waasi Goma zatimia, silaha zasalimishwa:MONUSCO

Saa 48 kwa waasi Goma zatimia, silaha zasalimishwa:MONUSCO

Kipindi cha saa 48 kilichotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kwa waasi na mtu yeyote mwenye silaha kusalimisha, kimetimia ambapo ujumbe huo umesema kuna kila dalili kuwa silaha zimesalimishwa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta)

Jumatano ya wiki hii kamanda mkuu wa MONUSCO Jenerali Carlos Alberto dos Santos Crus alitoa tangazo rasmi la kipindi cha saa 48 kwa waasi wa kundi la M23 na mtu yeyote mwenye silaha huko Goma, Mashariki mwa DRC kusalimisha silaha yoyote aliyo nayo kwani ni jeshi tu la DRC au walinda amani wa Umoja wa Mataifa wenye ndio wenye dhamana ya kubeba silaha.

 (SAUTI KAMANDA)

 Tangazo hilo limefikia ukomo wake leo saa Kumi kwa saa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo msemaji wa MONUSCO Carlos Araujo amesema hali ya usalama ni shwari na kipindi hicho kimemalizika kwa matumaini.

(SAUTI CARLOS)

Msemaji huyo licha ya kueleza kuwa ni mapema mno kutoa tathmini lakini dalili ni nzuri na kwamba MONUSCO na jeshi la serikali wataendelea na doria.

 (SAUTI YA CARLOS)