Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brigedi ya MONUSCO ya Kivu Kaskazini yapata mafunzo ya kurejesha amani na utulivu

Brigedi ya MONUSCO ya Kivu Kaskazini yapata mafunzo ya kurejesha amani na utulivu

Walinda amani 33 kutoka India wanao hudumu kwenye Brigedi ya kikosi cha MONUSCO huko Kivu Kaskazini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wanapatiwa mafunzo ya kurejesha amani na utulivu.Mafunzo hayo yaliyoanza wiki hii yatamalizika tareheTisa mwezi Agosti ambapo lengo ni kuwapatia stadi za kuwawezesha kukabiliana na ghasia za mijini huku wakizingatia haki za binadamu na uhuru wa raia.

Pindi wakishakamilisha mafunzo hayo wataungana na vikosi vya polisi kwenye eneo hilo ambavyo mara kwa mara vimekuwa vikikabiliana na matukio ya uvunjifu wa amani. Awamu ya pili ya mafunzo itaanza tarehe Tano hadi 16 mwezi ujao huko Sake, kilometa 27 kutoka Goma Magharibi.