Mauaji yaongezeka Afghanstan :UNAMA

31 Julai 2013

Ripoti mpya ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanstan, UNAMA, kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu inaonyesha kuwa idadi ya vifo vya raia imeongezeka ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(TAARIFA YA GRACE)

Kwa muibu wa Mkurugenzi wa haki za binadamu wa UNAMA Georgette Gagnon ripoti hiyo imeainisha kwamba idadi kubwa ya vifo vimetokana vifaa vya milipuko vinavyotumiwa na vikundi binafsi, imekariri vifo vya raia 1,319 na majeruhi 2533 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14 kwa vifo na asilimia 28 kwa majeruhi ikilinagnishwa na mwaka jana.

Sababu nyingine iloyotajwa kuchangia ongezeko hilo ni mapigano ya nchi kavu kati ya vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo na waasi wa serikali huku sababu nyingine ikiwa ni vifo vya kukusudiwa kutokana na mashambulizi yanayowalenga raia ambayo hufanywa na waasi.

(SAUTI GAGNON)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter