Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM apongeza uchaguzi wa Cambodia

Mtaalamu wa UM apongeza uchaguzi wa Cambodia

Mtaaalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadmu nchini Cambodia amesifu uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwishoni  mwa juma na ametaka kuwepo kwa hali ya utulivu na ustahimlivu wa kisiasa.Surya Subedi amesema kuwa uchaguzi huo wa jumapili iliyopita ni kielelezo cha ukomavu wa kisiasa na kusema kwamba wananchi wake wametumia vyema fursa ya utekelezaji wa misingi ya kidemokrasia.

Pamoja na kupongeza jinsi ya uchaguzi huo ulivyofanyika katika misingi ya amani na uhuru, lakini amewataka wanasiasa pamoja na wananchi kuendelea kuwa watulivu hasa wakati huu wakitekeleza jukumu la kuendesha mageuzi.

Ametaka pia kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kupalilia chuki za ukabila na amewahimiza kuendelea kulijenga taifa lao.