Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yatuma askari kuongeza ulinzi wa raia

MONUSCO yatuma askari kuongeza ulinzi wa raia

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, umewapa watu wenye silaha wasio askari wa jeshi la serikali ya DRC masaa 48 kusalimisha silaha zao au wapokonywe silaha hizo kwa nguvu ikiwa hawatafanya hivyo kufikia saa kumi alasiri Agosti mosi. Ujumbe wa MONUSCO umesema kuwa umepeleka askari zaidi walinda doria kwenye maeneo karibu na miji ya Goma na Sake ili kuimarisha ulinzi wa raia katika miji hiyo na maeneo jirani.

Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa leo, MONUSCO imesema inachukulia watu wowote wenye silaha wasio askari wa vikosi vya kitaifa vya usalama kuwa tishio kwa usalama wa raia, na hivyo, itawapokonya silaha ili kudumisha eneo salama la kuwalinda raia katika maeneo yanayokaliwa na zaidi ya watu milioni moja mjini Goma na Sake. Kwenye barabara kati ya miji hiyo miwili pia kunapatikana kambi za wakimbizi wa ndani za Mugunga, wanapokaa wakimbizi 70,000 wa ndani walokimbia machafuko.

Tangu mwezi Mei, eneo hilo limeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa waasi wa M23 dhidi ya jeshi la taifa, FARCD, katika majaribio ya kuiteka miji ya Goma na Sake.

Katika mashambulizi hayo yaloanza mnamo Julai 14, M23 walitumia silaha zisizolenga shabaha kiholela, zikiwemo silaha nzito nzito, na hivyo kusababisha vifo vya raia. Waasi hao wa M23 pia wamelenga vituo vya Umoja wa Mataifa katika mashambulizi yao.

MONUSCO imesema kuongeza nguvu za eneo la usalama kutaondoa tishio la moja kwa moja kwa raia wa Goma na Sake.