Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kupambana na malaria zaleleta pamoja Shirika la msalaba mwekundu na wakfu wa UM

Juhudi za kupambana na malaria zaleleta pamoja Shirika la msalaba mwekundu na wakfu wa UM

Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Halali Nyekundu, IFRC, pamoja na Shirika la Msalaba Mwekundu la Tanzania na kampeni ya Wakf wa Umoja wa Mataifa ya Hakuna kingine ila vyandarua, leo yamezindua mkakati wa pamoja wa kuhakikisha vyandarua vya kudumu vilivyotiwa dawa ya kuua mbu vinasambaziwa zaidi ya wakimbizi  sitini na nane elfu kwenye kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania. Alice Kariuki na taarifa kamili(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

 

Uzinduzi huo ni sehemu ya mkakati wa Shirika la msalaba mwekundu nchini Tanzania linalosaidiana na mashirika mengine ya kihisani kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa malaria kwenye maeneo yaliyopo makambi ya wakimbizi.

Miongoni  mwa walioshiriki kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye kambi ya Nyarugusu iliyoko Mkoani Kigoma magharibi mwa Tanzania ni pamoja na Stephen Curry,kutoka chama cha Basketi nchini Marekani NBA

Curry amechangia vyandarua kadhaa vilivyonyunyiziwa dawa ambayo ina uwezo wa kudumu kwa muda mrefu. Ugonjwa wa Malaria unaelezwa kusababisha vifo katika maeneo mengi ya kambi za wakimbizi huku wanawake wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wakiathirika zaidi na tatizo hilo.

 Akizungumzia kampeni hiyo, Rais wa chama cha msalaba mwekundu nchini Tanzania Dk.George Nangale alisema kuwa pamoja na kusambaza vyandarua hivyo, lakini pia kampeni hiyo inakwenda sambamba na utoaji elimu juu ya namna ya kukabiliana na mbu wasambazao ugonjwa huo.