Unyanyasaji wa kingono katika jimbo la kivu kaskazini, DRC umeongezeka:UNHCR

30 Julai 2013

Mapigano ya mara kwa mara katika jimbo la Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC yanawalazimu raia wengi zaidi kuhama makwao na kuwatia wanawake, wasichana na hata wanaume katika hatari ya kubakwa, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR. Joseph Msami na taarfia zaidi. (TAARIFA YA JOSEPH MSAMI)

Uchunguzi uliofanywa na timu ya wataalamu kutoka UNHCR umebaini kuwepo ongezeko kubwa la matukio ya unyanyasaji wa kingono na kwamba katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari mwaka huu jumla ya visa 705 zimerekodiwa ikiwemo matukio 619 ya ubakaji.

UNHCR inasema kuwa waathirika wa matukio hayo ni pamoja na makundi ya watoto wapatao 288, na wanaume 43 na kuongeza watendaji wa matukio hayo ni askari wenye silaha. Fatoumata Lejeune-Kaba ni msemaji wa  UNHCR

 (SAUTI YA FATOUMATA)