Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yakaribisha uamuzi wa mahakama kuu ya Kenya wa kuzuia kutimuliwa kwa wakimbizi mijini

UNHCR yakaribisha uamuzi wa mahakama kuu ya Kenya wa kuzuia kutimuliwa kwa wakimbizi mijini

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limekaribisha uamuzi wa mahakama kuu nchiniKenyaya kudumisha haki ya kuishi mijini kwa wakimbizi walio mijini. Uamuzi huu wa mahakama unatolewa kutokana  na kesi iliyowasilishwa mahakamani ya kupinga amri iliyotolewa na serikali yaKenyamwezi Disemba ya kutaka wakimbizi wote walio mijini kuhamishiwa kwenye kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma. Grace Kaneiya na maelezo zaidi. (TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Mahakama kuu ilipinga amri hiyo ambayo ingekuwa yenye athari nyingi kwa jamii za wakimbizi zilizo mjini Nairobi na miji mingine nchini Kenya. Baada ya kutolewa kwa uamuzi huo wa mahakama wakimbizi wengine hasa kutoka nchini Somalia pamoja na watafuta hifadhi waliripoti kuhangaishwa na polisi mjini Nairobi. Wengine hawataki kutembea wakihofia kuhangaishwa hali ambayo imesababisha wengi wao kurudi nchini Somalia au kuhamia mataifa mengine.

Wengi wa wakimbizi wanaoishi mijini wanategemea misaada ya kibinadamu. Hadi mwezi Disemba mwaka uliopita kulikuwa na jumla ya wakimbizi 51,000 wanaoishi mijini nchini Kenya.