Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani vikali shambulizi kwenye jengo la Waturuki Somalia

Ban alaani vikali shambulizi kwenye jengo la Waturuki Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelaani vikali shambulizi la kigaidi lililotekelezwa dhidi ya ofisi ilokaliwa na wafanyakazi wa kituruki mjini Mogadishu.

Bwana Ban ametuma risala za rambirambi kwa serikali na watu wa Uturuki, na kwa watu wa Somalia.

Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amesema Uturuki ni mshirika muhimu kwa serikali ya Somalia, na inajaribu katika mazingira magumu kuwasaidia raia wa Somalia katika juhudi zao za kutafuta amani, utulivu na maendeleo.

Amesema mashambulizi ya kigaidi ya aina hiyo yasiwazuie washirika wa Somalia au kuvunja ari yao ya kusimama bega kwa bega na serikali ya Somalia na watu wake.