Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa UM akaribisha kuachiwa huru kwa wafungwa, huku akielezea hofu yake kufuatia wanaokamatwa

Mtaalam wa UM akaribisha kuachiwa huru kwa wafungwa, huku akielezea hofu yake kufuatia wanaokamatwa

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadam nchini Myanmar, Tomás Ojea Quintana, amekaribisha hatua ya msamaha wa rais wa nchi hiyo Julai 23 ambapo watu  73  walofungwa kwa kuwa na dhana tofauti  huku akielezea wasiwasi kufuatia kukamatwa kwa wanaharakati (TAARIFA YA GEORGE)

 Kuachiwa kwa wafungwa hao kumeelezewa na mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuwa ni matunda yatokanayo ya mchakato wa mageuzi yanayoendelea sasa katika taifahilo.

Mtaalamu huyo Ojea hata hivyo ameelezea wasiwasi wake  kutokana na kamata kamata inayoendelea ambayo inakwenda sambamba na watu kutupwa gerezani.

Kumekuwa na madai kuwa msaka huo unachagizwa na mitazamo ya kisiasa na kwamba, wengi wanaokamatwa wanawekwa kizuizini kwa mtaji wa kisiasa.

Akielezea zaidi hali hiyo, mtaaamu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa anaamini vitendo vya kuwasaka wanasiasa vingali vinaendelea na yeye anafuatilia kwa karibu matukio yote yanayoendelea kujiri na ataka kufahamu ukweli zaidi wa amambo wakati atapotembelea taifahilomwezi ujao.

Amesema kuna haja ya kufanyiwa marekebisho baadhi ya sheria ambazo ameziita kandamiza zikiwemo zile zinazobinya uhuru wa watu kukusanyika .