Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wenye matatizo ya ugonjwa wa ini wana haki ya kupata huduma bora za matibabu

Watu wenye matatizo ya ugonjwa wa ini wana haki ya kupata huduma bora za matibabu

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na madawa ya kulevya na uhalifu ametoa wito wa kuongeza juhudi ili kuzalisha mbinu na mikakati ya kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa ini huku akitaka kutolewa kwa matibabu sawa kwa mamia ya watu wanaathiriwa na matumizi ya madawa ya kulevya.Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya tatizo la ini duniani, Yury Fedotov amesema kuwa watu wanaokabiliwa na matatizo ya virusi visababishao ugonjwa huo wana haki ya kupatiwa matibabu na kuongeza kuwa mamlaka za dola zinawajibika kuweka mazingira mazuri ya utoaji matibabu hayo.

Ugonjwa wa manjano husababishwa na virusi ambavyo  baadaye huathiri maini na hata kumsababishia kifo mtu. Takwimu zinaonyesha kwamba  kiasi cha watu milioni 1.4 duniani kote hupoteza maisha  kila mwaka kutokana na tatizo hilo la maini.

Virusi hivi vimegawika katika makundi kuanzia A mpaka E na inaelezwa kwamba virusi aiana C ndiyo hatari zaidi kwa maisha ya binadamu.