Shirika la la OzHarvest lashirikiana na UNEP kuwalisha watu 5000 mjini Sydney

29 Julai 2013

Jinsi ambavyo wanadamu wanavyotumia chakula chao ni ishara kuwa watu katika Karne hii ya 21 si waangalifu na hawafanyi jitihada za kukilinda huku karibu theluthi moja ya chakula kinachozalishwa kikitupwa. Kwa mara ya kwanza kabisa nchini Australia OzHarvest kama mshirika mkuu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP nchini Australia lililo kwenye kampeni ya kuzuia utupaji wa chakula hii leo liliandaa shughuli ya kimataifa yenye kauli mbiu kuwalisha watu 5000 katika eneo la Martin mjini Sydney.

Baadhi ya wapishi wakubwa nchini humo na mamia ya watu wakujitolea walijiunga na Shirika la OzHarvest kuwapakulia watu chakula moto cha mchana ambacho kimeokolewa na ambacho badala yake kingetupwa. Chakula cha gharama ya dola billioni 7.8 hutupwa nchini Australia zikiwa ni tani milioni nne kila mwaka au mfuko mmoja kwa kila mifuko mitano ya chakula kinachonunuliwa. Kuwalisha watu 5000 kunaashiria jinsi ilivyo rahisi katika kupunguza chakula kiwachotupwa na jinsi watu wa kawaida , wazalishaji na maduka ya jumla na serikali zinavyoweza kufanya kupunguza utupaji wa chakula.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter