Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM awataka viongozi wa kisiasa Iraq kukomesha machafuko:

Mwakilishi wa UM awataka viongozi wa kisiasa Iraq kukomesha machafuko:

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa mataifa nchini Iraq ameelezea hofu yake kufuatia wimbi jipya la milipuko ya mabomu yaliyotegwa kwenye gari lilozuka Jumatatu na kusababisha vifo vya watu kadhaa na kujeruhi wengine.Afisa huyo ambaye ni kaimu mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq bwana Gyorgy Busztin amesema kinachomtoa mashaka makubwa ni kuongezeka kwa kiwango cha machafuko ambayo yanaiweka kwenye hatihati nchi hiyo ya kurejea tena kwenye wimbi la machafuko ya kidini.

Mwakilishi huyo amesema Iraq inavuja damu kutokana na machafuko yalotapakaa kila kona ambayo kwa bahati mbaya yamefikia kiwango cha juu kabisa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Amewataka viongozi wa pande zote za kisiasa kuchukua hatua mara moja za kukomesha umwagaji damu unaondelea.