Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yalaani ukatili unaofanywa na kikundi cha m23

MONUSCO yalaani ukatili unaofanywa na kikundi cha m23

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC umeelezea wasiwasi wake juu ya madai ya kwamba kikundi cha waasi cha M23 kinahusika na mauji, utumikishaji wa lazima wa raia kwenye kikundi hicho na hata kukamata raia. Taarifa ya Jason Nyakundi inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Jason)

Kufuatia hali hiyo Gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Julien Paluku ametaka mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu, ICC kuingilia kati hali ilivyo jimboni kwake ili sheria ichukue mkondo wake.