Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yakabiliwa na uhaba wa fedha

IOM yakabiliwa na uhaba wa fedha

Shirika la Uhamiaji duniani IOM linakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha jambo linalohataraisha kusimama kwa baadhi ya miradi inayofanywa na shirika hilo katika nchi mbali mbali ikiwemo ya kuwarudisha makwao wahamiaji, wakimbizi na kuwapatia huduma za kijamii. IOM inahitaji kiasi cha dola milioni mia mbili thelathini na tatu nukta mbili ili kutekeleza majukumu yake kikamilifu mwaka huu. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE)