Wakimbizi kutoka Syria wakamatwa nchini Misri

26 Julai 2013

Kaskazini mwa Afrika nchini misri ambapo Takriban Wasyria 85 wamekamatwa na kufungwa na jeshi nchini Misri kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.Jason Nyakundi na tarifa kamili. (TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Kati ya wale waliokamatwa ni watoto kadha na Wasyria ambao wameandikishwa na UNHCR nchini Misri. UNHCR inasema kuwa kuna upinzani unaozidi kushuhudiwa dhidi ya Wasyria nchini Misri huku baadhi ya wale wanaokamatwa wakishutumiwa kwa kuhusika kwenye maandamano na ghasia wakati ya kupinduliwa kwa serikali ya awali ya chama cha Muslim brotherhood.

Melissa Fleming kutoka UNHCR anasema kuwa dhuluma dhidi ya wasyria pia zimechochewa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Misri vinavyotangaza habari za kotopendeza dhidi ya Wasyria

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

“Tumekuwa tukiomba kukutana na wasyria 85 wanaozuiliwa hao ndio tunafahamu juu yao na tunauliza hakikisho kuwa hawatarejeshwa Syria. Tunasisitiza kuwa waweze kupata haki ya sheria nchini Misri. Misri ilikuwa moja ya nchi rafiki mkuu kwa Syria tangu kuanza kwa mzozo. Kwa miaka  kadha iliyopita serikali imekuwa ikitoa visa pamoja na ruhusa ya kutumia huduma za umma. Kile wanachotufahamisha wakati kama huu ni kwamba wanaogopa  kutoka nje wakisema huenda wakakamatwa. Pia tumafahamu kuwa wasyria zaidi wanajitokeza kujiandikisha na UNHCR.”

Serikali inakadiria kuwa raia waSyriawalio misri ni kati ya watu 250,000 na 300,000 ambapo kati ya hao 80,000 wamejiandikisha na UNHCR.

Wakati hayo yakijiri Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki Moon amesema anafuatilia kwa umakini hali ya kisiasa nchini Misri na kutaka pande zote kujitahidi kujizuia huku akisema anaunga mkono haki ya wananchi kuandamana kwa amani.