Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mamluki na makampuni ya ulinzi ya kibinafsi kujadili matumizi ya makumpuni kwenye shughuli za Umoja wa Mataifa
Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linalohusika na matumizi ya mamluki linatarajiwa kujadili kutumika kwa makampuni ya kibinafsi ya kutoa ulinzi kwenye shughuli za amani za Umoja wa Mataifa na kwenye utoaji wa huduma za kibinadamu. Mkutano wa kujadili suala hilo utaandaliwa tarere 31 mwezi huu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kama sehemu ya utafiti wa mwaka mzima kuhusu matumzi ya makampuni ya kibinafsi ya ulinzi ambayo matokeo yake yatawasilishwa mbele ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2014. Kama mtumiaji mkubwa wa huduma za usalama Umoja wa Mataifa una fursa kubwa kaweka viwango vipya kwenye sekta hiyo ili kuiwezesha kuafikia viwango vya kimataifa na katika kutekezwa kwa mikataba ya Umoja wa Mataifa.