Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yachukua hatua za kukabiliana na ugonjwa wa homa ya ini

Tanzania yachukua hatua za kukabiliana na ugonjwa wa homa ya ini

Ugonjwa wa ini ni miongoni mwa matatizo ambayo yanaendelea kuziandama nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo sasa zimeanzisha jitihada za kukabiliana nao kwa kutiwa shime na shirika la afya duniani WHO.

Ugonjwa huu ambao kwa baadhi wanautambua kama ugonjwa wa manjano, unaelezewa na Umoja wa Mataifa kama “ tatizo la kimya kimya” kwa maana kwamba, wengi wanaokumbwa na ugonjwa huo wanachukua muda kuutambua.

Kutokana na ukubwa wa tatizo hili, leo kwenye makala hii mwenzetu George Njogopa anaangazia hali ilivyo nchini Tanzania na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa, karibu uungane naye.

(MAKALA YA GEORGE NJOGOPA)