Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni maalum yazinduliwa kutetea mashoga

Kampeni maalum yazinduliwa kutetea mashoga

Ofisi ya tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imezindua kampeni ya kipeke ijulikanayo kama Huru na Sawa yenye lengo la kuelimisha umma juu ya haki sawa kwa mashoga, wasagaji na waliobadili jinsi zao. Uzinduzi huo umefanyika huko Cape Town, Afrika Kusini ambapo Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa NAvi Pillay amesema tako la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linatamka bayana kuwa kila mtu anazaliwa huru na sawa na anapaswa kuishi maisha ya staha bila kubaguliwa.

Bi. Pillay amesema hata hivyo bado suala hilo ni ndoto kwa mashoga, wasagaji na waliobadili jinsi kwani wanatengwa na kukumbana na chuki kila siku.

Amesema kubadili mtazamo si jambo rahisi lakini imewezekana kwa masuala mengine na ndivyo wanataka kuanza kampeni hiyo kupitia mashauriano duniani kote ambapo itahusisha marekebisho ya sheria na kuondoa chuki dhidi ya makundi hayo.

Katika mkutano huo Bi. Pillay aliungana pia na Askofu Mkuu Desmond Tutu na balozi wa hiari wa UNICEF kuhusu Malaria Yvonne Chaka Chaka.