Uingereza kupatia msaada wa fedha kituo cha kimataifa cha biashara

26 Julai 2013

Uingereza imetangaza msaada wa zaidi ya dola Milioni Kumi kwa ajili ya kituo cha kimataifa cha biashara, ITC kwa lengo la kuboresha uwezo wa kibiashara kwa nchi zinazoendelea. Grace Kaneiya na maelezo zaidi. (Ripoti ya Grace)

Kiasi hicho cha fedha ambacho kimepangwa kutumika kwa kipindi cha miaka mitatu, kitasaidia kufungua njia za kibishara kwa kuondosha vizingiti vilivyokuwa vikikwamisha ufanyaji biashara katika nchi zinazoendelea.

Kutolewa kwa fedha hizo pia kunatazamia kutoa fursa kwa wajasiriamali wanawake kujitokeza kwenye duru za kimataifa. Pamoja na kwamba viwango vya ushuru wa forodha vimeendelea kushuka chini, lakini  kukosekana kwa mbinu bora za kukabiliana na viwango hivyo vya ushuru wa forodha kumefanya hali ya upelekaji bidhaa katika masoko ya ndani na yale ya nje kuwa ya nchini.

Hali hiyo imefanya wajasiriamali wengi wanawake kuathirika na hivyo kushindwa kufanya vyema kwenye biashara za kimataifa. Jarle Hetland ni msemaji wa ITC

(SAUTI YA JARLE HETLAND)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud