Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa umeimarisha stadi za wakaguzi kutoka Tanzania: Uttouh

Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa umeimarisha stadi za wakaguzi kutoka Tanzania: Uttouh

Mapema wiki hii wajumbe wa bodi ya ukaguzi wa Umoja wa Mataifa walikutana mjini New York Marekani ambapo pamoja na mambo mengine walitia saini ripoti za ukaguzi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka wa fedha 2012. miongoni mwa wajumbe hao ni Ludovick Uttouh, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali yaTanzania. Katika mahojiano na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Uttouh alielezea kile walichofanya na fursa ya Tanzania katika bodi hiyo, kwanza anaanza kwa kuelezea kile kilichowaleta New York.