Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay alaani vikali mauaji ya kiongozi wa upinzani nchini Tunisian

Pillay alaani vikali mauaji ya kiongozi wa upinzani nchini Tunisian

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amelaani vikali mauaji ya leo Alhamisi ya mwanasiasa wa upinzani nchini Tunisia na kuwataka watu wan chi hiyo na wanasiasa kuungana kupinga majaribio ya kusambaratisha mchakato wa kipindi cha mpito cha kidemokrasia nchini humo.

Mohamed Brahmi, mbunge, alipigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yake kwenye viunga vya Tunis Alhamisi asubuhi wakati binti yake akiwepo Pillay amesema ameshitushwa na kuhuzunishwa na habari za mauaji ya Bwana Brahmi.

Bi Pillay ameutaka uongozi wa Tuniasia kuanza uchunguzi wa wazi mara moja na kuhakikisha waliotekeleza mauaji hayo wanwajibishwa. Ameongeza kuwa hii ni mara ya tatu mauaji ya aina hiyo yanafanyika katika kipindi cha miezi 10. Bwana Lotfi Naghdh aliuawa Oktoba 2012 na miezi sita tuu iliyopita mwanasiasa mwingine Chokri Belaid, aliuawa katika mazingira kama ya Brahmi na uchunguzi dhidi ya mauaji ya Belaid haujakamilika wala mazingira aliyouawa kutanabaishwa.

Pillay amesema mauaji ya Brahmi, ambayo yanakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 56 tangu kuundwa taifa la Tunisia yanaweka hatarini mchakato muhimu wa katiba ambao upo katika hatua za mwisho.

Amewataka wadau wote, serikali, wapinzani, jamii na jumuiya za kijamii kusimama imara na kwa sauti moja na kutetea uhuru wa kila mmoja wa kujiunga na kuelezea mitazamo yao ya kisiasa.