Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aitaka Israel kutupilia mbali sheria inayolenga kuhamisha watu wa jamii ya Bedoui

Pillay aitaka Israel kutupilia mbali sheria inayolenga kuhamisha watu wa jamii ya Bedoui

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay  ameitaka serikali ya Israel kuufanyia mabadiliko msuada wa sheria ambao ikiwa utatekelezwa utasababisha kubomolewa kwa hadi vijiji 35 kwenye jangwa la Negev na kutwaliwa kwa ardhi ambapo huenda watu 30,000 hadi 40,000 kutoka jamii ya Bedouin wakatimuliwa kutoka kwa ardhi ya mababu zao. Jason Nyakundi na ripoti kamili.(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Pillay anasema kuwa kama raia yeyote wa Israel watu wa jamii ya Bedoui wana haki sawa ya kumiliki mali, nyumba na wapate huduma za umma kama jamii yeyote ile nchini Israel. Pillay alielezea masikikitiko yake kuwa bado serikali ya Israelinaendelea kuwalazimu raia wake wenye asili ya kiarabu kuhama makwao hata baada ya kulizungumzia suala hiloalipofanya ziara rasmi nchini Israelmiaka miwili iliyopita. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Pillay ameongeza kuwa ikiwa msuada huo utakuwa sheria utachochea kubomolewa kwa makao ya jamii hiyo na kuwalazimu watu hao kuhama makwao hatua ambayo itawanyima hakiyaoya kumiliki ardhi.