Mafuriko Mashariki mwa DPRK yaacha wengi bila makazi.

25 Julai 2013

Mvua kubwa za msimu huko Jamhuri ya kidemokrasia ya watu waKorea, DPRK zilizonyesha wiki mbili zilizopita zimesababisha mafuriko kwenye maeneo mengi nchini humo hususan maeneo ya kaskazini na kusini mwa mji mkuu Pyongyangna mamia hawana makazi. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi. (TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Kumekuwa na taarifa zinazopishana kuhusiana na idadi ya watu waliojeruhiwa kwenye mafuriko hayo ambayo yamesababisha kati ya watu 8 hadi 24 kupoteza maisha huku wengine 14 wakiwa hawajulikani waliko .

Katika tathmini yake ya awali serikali imesema kuwa kumekuwa  na uharibifu mkubwa wa majumba pamoja na mifumo ya miundombinu.

Ripoti zinasema kuwa kiasi cha watu 45,948 wamekosa makazi  na hali ni mbaya zaidi katika majimbo yaliyoko Kusin na Kaskazini mwa Pyonang.

Pia mafuriko hayo yameharibu mashamba na inakadiriwa kwamba kiasi cha hekari 1,000 za mavuno zimeharibiwa.Umoja wa Mataifa umetuma wataalamu wake kwa ajili ya kufanya tathmini.