Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wamaliza malipo ya fidia kwa Kuwait

Umoja wa Mataifa wamaliza malipo ya fidia kwa Kuwait

Tume ya kulipa fidia ya Umoja wa Mataifa imeipatia Kuwait zaidi ya dola Bilioni Moja ikiwa ni kiasi kilichokuwa kimebakia cha madai yake kufuatia uvamizi uliofanywa naIraq. George Njogopa anaripoti (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Hadi sasa kamishna hii tayari imeshatoa fidia kiasi cha dola za Marekani billion 42.3 ambazo ni kati ya dola bilioni 52.4 zilizotengwa kwa ajili ya fidia kwa serikali mbalimbali pamoja na mashirika ya kimataifa.

Fedha hizo zinatolewa kwa walalamikaji wanaofikia milioni 1.5 ambao malalamikoyaoyalikidhi vigezo. Hata hivyo bado  kuna kiasi kingine cha dola bilioni 10.1  hakijatolewa na kamishana hiyo.

Kundi ambalo bado halijapata fidia ni  lile la kundi E ambalo malalamiko yake yaliwasilishwa na serikali ya Kuwait kwa niaba ya kampuni ya Petrol ya nchini humo.

Katika mwaka 2000 walalamikaji walilipwa kiasi cha dola bilioni 14.7 kama fidia kutokana na shughuli za uzalishaji wa nishati ya mafuta kuharibu ardhi yaKuwait.

---