Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani DRC na nchi za maziwa makuu yaangaziwa

Amani DRC na nchi za maziwa makuu yaangaziwa

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo kujadili mustakabali wa amani katika ukanda wa nchi za maziwa makuu na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.Taarifa zaidi na Flora Nducha

(SAUTI YA FLORA NDUCHA)

Mkutano huo wa leo unakuja takribani miezi mitano baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani, usalama na ushirikiano ambapo mkutano wa leo utaangazia utekelezaji wa mkataba huo.

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi ni miongioni mwa wanadiplomasia watakaotoa mada katika amkuatno huo

(SAUTI MANONGI)

Je ujumbe wa Tanzania nchi ambayo imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kukuza amani ya ukanda huo ninini?

(SAUTI MANONGI)

Mkutano wa baraza la usalama pia utajadili ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utekelezaji wa mkataba wa amani DRC na ukanda mzima wan chi za maziwa makuu.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon leo amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry ambapo pamoja na kuzungumzia suala la Syria, aligusia pia amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

(SAUTI YA BAN)