Ripoti za ukaguzi wa mahesabu ya Umoja wa Mataifa zatiwa saini

25 Julai 2013

Bodi ya ukaguzi ya Umoja wa Mataifa imeridhia na kutia saini ripoti 15 za ukaguzi wa mahesabu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka wa fedha 2012. Hatua hiyo imefanyika wakati wa kikao cha bodi hiyo mjini New York, Marekani kinachojumuisha wadhibiti na wakaguzi wakuu wa mahesabu ya serikali kutoka Tanzania, Uingereza na China ambazo ndio wanachama wa bodi hiyo kwa sasa ambapo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kutoka Tanzania Bwana Ludovick Uttouh amesema kilichomo ndani ya ripoti hizo kitawekwa bayana mwezi Septemba mwaka huu.

(SAUTI UTTOUH-1)

Bwana Uttouh akaelezea jinsi Tanzania ilivyonufaika na ujumbe wa bodi hiyo.

(SAUTI YA UTTOUH-2)

Mahojiano zaidi na Bwana Uttouh yatapatikana kwenye ukurasa wetu.