Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yasema virusi vya homa ya ini "ni tatizo la kimya kimya"

WHO yasema virusi vya homa ya ini "ni tatizo la kimya kimya"

Shirika la afya ulimwenguni WHO limezitaka serikali duniani kutilia uzito juu ya virusi aina tano ambavyo vinasabisha tatizo la manjano na baadaye kuathiri maini. Inaelezwa kwamba kiasi cha watu milioni 1.4 duniani kote hupoteza maisha  kila mwaka kutokana na tatizo hilo la maini Taarifa zadi na Grace Kaneiya

(TAARIFA YA GRECE KANEIYA)

Wataalamu wa afya wanasema kuwa miongoni mwa virusi hivyo hasa vile vya aina B na C vinauwezo mkubwa wa kusababisha matatizo sugu na hatimaye kuzalisha kansa ya ini.

Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kuwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa manjano vinachukuliwa kama “ tatizo la kimya kimya” kwani idadi kubwa ya watu hawatambui kama wameambukizwa na virusi hivyo na baada ya kupita miongo mingi ndipo wanapojikuta wanatumbukia kwenye matatizo ya ini.

WHO ambayo inatazamia kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini hapo Julai 28, imehimiza juu ya kile ilichokiita kuendelea kuongeza hamasa kwa wananchi ili wautambue vizuri ukubwa wa tatizo hilo na hatimaye kuleta mafanikio.Dr Stefan Wiktor kutoka WHO anahusika na mradi unaongazia ugonjwa huo.

(SAUTI YA DR STEFAN WIKTOR)

“Tunaona kwamba ni muhimu kwa nchi kuwa na mipango na kuanzisha vitengo vitakavyokuwa na jukumu la kushughulika na tatizo la ugonjwa wa manjano. Tulipoziuliza nchi, asilimia 38 zilisema kuwa tayari zilishaweka mipango mikakati ya kitaifa lakini ni asilimia 29 ndizo zilizokuwa na vituo maalumu kwa ajili ya tatizo hili.

Tunaendelea kufanya kazi na nchi ili kuzisaidia kuendeleza na kutekeleza mipango ya kitaifa kuhusiana na ugonjwa huu wa homa ya ini.

Kumekuwa na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika eneo la kuzuia ugonjwa huo na hii ni katika eneo la utoaji kinga kukabili homa ya ini  B.