Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya ukame yaweza kusababisha uhamiaji, IOM yachukua hatua

Hali ya ukame yaweza kusababisha uhamiaji, IOM yachukua hatua

Mapema mwaka huu visiwa vya Marshall huko kwenye bahari ya Pasifiki vilikumbwa na ukame mkubwa na kusababisha watu kutafuta mbinu mbadala za kupata chakula. Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limechukua hatua kusaidia vyakula na vifaa vingine muhimu maelfu ya wakazi haokamanjia mojawapo ya kudhibiti uhamiaji wakati huu ambapo wananchi hao wanasubiri mavuno. Katika mahojiano kwa njia ya simu nami Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa, msemaji wa IOM Jumbe Omari anazungumzia misaada waliyotoa huku akigusia uhusiano kati ya uhamiaji na mabadiliko ya tabia nchi hata katika nchi za Mashariki mwa Afrika. Kwanza anaanza kwa kusema hali ilivyokuwa hadi wakaamua kutoa misaada huko visiwa vyaMarshall.