Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yafanikiwa kuwasilisha misaada muhimu kwa watoto huko Aleppo

UNICEF yafanikiwa kuwasilisha misaada muhimu kwa watoto huko Aleppo

Hatimaye Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na washirika wake wamefanikiwa kukamilisha usambazaji wa vifaa muhimu vya misaada kwa watoto na familia zao kwenye mji wa Aleppo, Kaskazini Magharibi mwa Syria unaokabiliwa na vuta ni kuvute ya mapigano kati ya serikali na waasi.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Yoka Brandt ambaye alikuwepo eneo hilo amesema misaada hiyo imefika wakati muafaka kwa kuwa hali ya kibinadamu huko Aleppo ni mbaya.

Misaada iliyopelekwa ni pamoja na vikasha vya dawa dhidi ya kipindupindu kwa ajili ya wagonjwa Elfu Thelathini, vifaa tiba kwa watu Elfu Ishirini na vikasha Elfu Mbili vyenye vifaa vya kujisafi bila kusahau majiko ya kupikia, vifaa vya shule na biskuti zenye virutubisho.

Yoka amesema lengo ni kufikia watoto ambao wana mahitaji zaidi billa kujali maeneo waliko. Aleppo ni eneo lenye idadi kubwa ya wahanga wa mzozo unaoendelea nchini Syria ikiwa na watu takribani Milioni Milioni Mbili nukta nne, nusu yao wakiwa ni watoto