Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabunge mengi hayana mamlaka ya kuidhinisha mikopo:IPU

Mabunge mengi hayana mamlaka ya kuidhinisha mikopo:IPU

Karibu asilimia 40 ya mabunge hayana mamlaka ya kuidhinisha mikopo inayoombwa na serikali kutoka kwa mashirika ya kifedha ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia na Shirika la fedha duniani IMF kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chama cha kimtaifa cha wabunge na benki ya dunia. Wakati huo huo karibu theluthi mbili au asilimia 64 ya wabunge wanasema kuwa hawashiriki kwa vyovyote vile katika kuidhiniswa kwa mkopo wowote kwa serikali. Ripoti hiyo inayashirikisha mataiafa 100 yanayoendelea. Jemini Pandya ni mmsemaji wa IPU.

(SAUTI YA  JEMIN PANDYA)