Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaanzisha oparesheni ya kuwafikia waliokimbia makwao kutokana na ghasia nchini Sudan Kusini

WFP yaanzisha oparesheni ya kuwafikia waliokimbia makwao kutokana na ghasia nchini Sudan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limezindua oparesheni inayoshirikisha matumizi ya ndege aina ya helkopta katika kuwapelekea misaada ya chakula cha dharura maelfu ya watu ambao wamekimbia mapigano kwenye kaunti ya Pibor iliyo kwenye jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini. Mapigano kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo yakiwemo mapigano mapya kati ya jamii za Lou Nuer na Murle yamewalazimu maelfu ya watu kwenye maeneo ambayo hayafikiki kutokana na kuwepo na barabara duni na ukosefu wa usalama. Elisabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)