Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera ya wakimbizi wa ndani Yemen yakaribishwa na UNHCR

Sera ya wakimbizi wa ndani Yemen yakaribishwa na UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua ya serikali ya Yemen ya kupitisha sera ya kitaifa kuhusu wakimbizi wa ndani.Serikali ya nchi hiyo imeidhinisha sera hiyo mwishoni mwa Juni . Sera hiyo ina lengo la kuwalinda Wayemen zaidi ya 500,000 ambao wamelazimika kuzikimbia nyumba zao katika miaka ya karibuni .

Pia ina nia ya kuisaidia serikali kutatua tatizo la wakimbizi wa ndani katika taifa hilo la Ghuba. Kwa mujibu wa UNHCR hii ni hatua kubwa kwa serikali ya Yemen kwa mikakati ya kusonga mbele baada ya machafuko.