Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yanayoendelea mashariki mwa DR Congo yatia hofu

Machafuko yanayoendelea mashariki mwa DR Congo yatia hofu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa mashaka na kuendelea kwa hali ya machafuko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Kwa mujibu wa UNHCR Jumapili iliyopita milipuko ya mabomu na milio ya risasi iliyokuwa ikirindima kutoka upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilisikika hadi kwenye eneo la mpkani la Mashariki mwa Uganda.

Hali hiyo imesababisha wakimbizi kuvuka mpaka hadi nchi jirani na UNHCR inaamini kwamba wengi zaidi watakuwa wanajaribu kuvuka lakini wanashindwa kutokana na sababu mbalimbali.