Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yalopita si ndwele, tugange yajayo: Rais Kikwete

Yalopita si ndwele, tugange yajayo: Rais Kikwete

Nchini Tanzania walinzi amani Saba waliouawa kwenye shambulio la kuvizia hukoDarfur, Sudan tarehe 13 mwezi huu wameagwa katika shughuli ya kitaifa ya maombolezo.Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Rais Jakaya Kikwete aliongoza shughuli hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya waombolezaji wakiwemo wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, serikali ya Tanzania na mabalozi bila kusahau wananchi. Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa alihudhuria shughuli hiyo na kutuletea taarifa kama ilivyoandaliwa na Assumpta Massoi.