Uungwaji mkono ukeketaji watoto wa kike na wanawake wapungua: UNICEF

22 Julai 2013

Idadi kubwa ya wakazi wa nchi ambako ukeketaji wanawake na watoto wa kike hufanyika wanapinga kuendelea kufanyika kwa kitendo hicho na hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iliyotolewa Jumatatu. Flora Nducha na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Matokeo ya ripoti hiyo yanatokana na tafiti zilizochukuliwa kwenye mataifa 29 ya Afrika na Mashariki ya Kati kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 juu ya ukeketaji ambapo nchini Kenya asilimia 59 ya wasichana na wanawake waliokeketwa wamesema hawaoni manufaa ya kitendo hicho huku nchini Nigeria asilimia 35 ya wavulana na wanaume pamoja na asilimia 31 ya wasichana na wanawake wanasema hawafahamu fikra za jinsia nyingine juu ya kitendo hicho. Nchini Tanzania ripoti yaonyesha kuwa hatari ya kukeketwa ni kubwa kwa wanawake walio na umri kati ya miaka 45 na 49 kuliko wasichana wa kati ya miaka 15 na 19. Lakini cha kutia moyo kwa mujibu wa Fransesca Monetti mtaalamu kutoka UNICEF ni kwamba…....

(SAUTI YA MONETI)

Hata hivyo UNICEF inasema licha ya kuporomoka kuungwa mkono kwa ukeketaji bado mamilioni ya wasichana wako hatarini hivyo ni vyema kuchochea kampeni za kutokomeza fikra potofu zinazoeneza kitendo hicho.