Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya sheria kuhusu haki maeneo ya kazi yaanza kutekelezwa nchini Bangladesh

Mabadiliko ya sheria kuhusu haki maeneo ya kazi yaanza kutekelezwa nchini Bangladesh

Mabadiliko kwenye sheria ya kazi ya mwaka 2006 nchini Bangladesh iliyoanza kutekelezwa tarehe 15 mwezi huu ni moja wapo ya sehemu ya kutimiszwa kwa ahadi ya serikali ya kuheshimu haki ya uhuru wa kushauriana na kushughulia zaidi masula ya usalama kazini na afya. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Mabadiliko hayo yaliyofanywa na viwango vya kimataifa yanatakaguliwa na Shirika la kazi duniani ILO baadaye mwaka huu. Ukaguzi wa hapo awali unaonyesha kuwa mabadilio hayo yametekeleza matakwa ya ILO lakini hata hivyo yana upungufu kadha wa kuafikiwa kwa viwango vilivyowekwa na ILO. Masuala kadha ya kuboresha usalama kwenye maeneo ya kazi yamejumuishwa kwenye sheria hiyo. Hata hivyo ILO bado haijapokewa tafsiri yoyote ya nakala ya mwisho ya mabadiliko hayo. Masuala kadha ambayo yamekuwa yakiwanyima wafanyikazi uhuru wa kushauriana ambayo yamekuwa yakiangaziwa zaidi na ILO hayakushughulikiwa na mabadiko hayo. Kati ya hayo ni kuunguzwa asilimia 30 ya watu wa chini zaidi wanaohitajika kubuni chama. Hata hivyo ILO inasema kuwa hatua zimepigwa na serikali miezi ya hivi majuzi katika kuandikisha vyama hatua ambazo hazikuhitaji mabadiliko ya sheria.