Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maradhi ya moyo yasalia kuwa muuaji namba moja:WHO

Maradhi ya moyo yasalia kuwa muuaji namba moja:WHO

Shirika la afya duniani WHO limesema maradhi ya moyo yanasalia kuwa chanzo namba moja cha vifo duniani ikiwa ni moja ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.Maradhi hayo yamekatili maisha ya watu karibu milioni 17 mwaka 2011 ikiwa ni sawa na watu 3 kati ya kila vifo 10. WHO inasema watu milioni 7 katiyaohufa na maradhi ya kawaida ya moyo na wengine milioni 6.2 kufa kwa kiharusi.

Kwa ujumla magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs yamekuwa chanzo cha vifo theluthi mbili duniani mwaka 2011 ikiwa ni ongezeko la asilimia 60 kutoka mwaka 2000. Maradhi makubwa manne yasiyo ya kuambukiza ni ya moyo, saratani, kisukari na maradhi ya mapafu.