Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa DRC nchini Tanzania kupatiwa vyandarua kujikinga na Malaria

Wakimbizi wa DRC nchini Tanzania kupatiwa vyandarua kujikinga na Malaria

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na chama cha msalaba mwekundu nchini Tanzania umepanga kusambaza vyandarua kadhaa kwa  wakimbizi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC waliko katika kambi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma, kaskazini mwaTanzania. Mpango huo ambao pia unaungwa mkono na chama cha kimataifa cha msalaba mwekundu umelenga kukabiliana na tatizo la Malaria ambalo linatakwa kuongezeka katika eneo hilo.George Njogopa na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA GEORGE)

Mpango huo ambao umepangwa kutekelezwa mwishoni mwa mwezi huu umewalenga wakimbzi zaidi ya 68,000 waliko kwenye kambi hiyo na utatekekezwa sambamba na utoaji elimu kuhusiana na tatizohiloambalo linagharimu maisha ya watu 700,000 kila mwaka duniani kote.Kulingana na Mwenyekiti wa chama cha msalaba mwenkundu nchini Tanzania Dkt. George Nangale, kutolewa kwa vyandarua hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo hilo.Ilikufanikisha mpango huo, kila wakimbizi wawili watapatiwa chandarua kimoja.