Wananchi wa Burundi wamuenzi Mandela kwa msaada wake

19 Julai 2013

Mnamo tarehe 18 Julai wiki hii, ulimwengu mzima uliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mandela, ili kumuenzi Nelson Mandela, rais wa zamani wa Afrika Kusini na Shujaa wa kupigania uhuru na haki za binadamu.

Hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, ilifanyika hafla maalum ya kuadhimisha siku hiyo kwenye ukumbi wa mikutano ya Baraza Kuu, ambako Mandela amesifiwa kwenye hotuba mbali mbali, zilizotolewa na watu kama Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, mwanaharakati wa haki za binadamu Mchunganji Jesse Jackson, pamoja na mzee Andrew Mlangeni, aliyefungwa na Mandela kwenye kisiwa cha Robben na ambaye hadi sasa ni rafiki yake mkubwa.

Mzee Nelson Mandela anafahamika sio tu kama shujaa katika vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini mwake, bali pia katika juhudi za usuluhishi. Moja wapo ni katika nchi ya Burundi.

Taifa hilo ambalo lilitikiswa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya muongo mmoja linamchukulia Mzee Mandela kama muokozi baada ya juhudi zake zilizoshuhudia Mkataba wa Amani na Maridhiano wa Arusha wa mwaka 2000. Mkataba huu ndio umekuwa uti wa mgongo wa taifa hilo la Burundi baada ya kukomesha mgogoro kati ya wahutu na watutsi.

Kutoka Bujumbura, Muandishi wetu Ramadhani KIBUGA ametuandalia makala hii.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter