Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na ripoti za mapigano ya kikabila Guinea

Ban asikitishwa na ripoti za mapigano ya kikabila Guinea

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea kusikitishwa na ripoti za mapigano ya kikabila kusini mwa Guinea, ambayo yamesababisha vifo vingi na watu kupoteza mali zao.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wake, Bwana Ban ametoa wito wa utulivu na kuwataka watu wa Guinea kujiepusha na vitendo vyote ambavyo huenda vikazorotesha amani na utangamano miongoni mwa jamii na haki za binadamu.

Ametoa wito kwa viongozi wa kitaifa na kijamii kuhakikisha usalama wa watu na mali, na kuendeleza uongozi wa kisheria na kuandama mkondo wa mazungumzo kwa ajili ya kukabiliana na vitu vinavyozua ugomvi miongoni mwa jamii mbalimbali. Amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira bora kwa uchaguzi wa amani na kidemokrasia mnamo Septemba 24, kama ilivyopangwa.