UNHCR yafanya jitihada za kuwasiadia wakimbizi kutoka DRC walio nchini Uganda

19 Julai 2013

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linafanya jitihada za kuwapelekea mahitaji muhimu wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC. Wakimbizi hao walianza kukimbia makwao tarehe 11 mwezi Julai baada ya uvamizi uliofanywa kweneye eneo la Kamango mashariki mwa DRC. Jason Nyakundi anaripoti. 

(Taarifa ya Jason)

UNHCR inasema kuwa juma moja baada ya wakimbizi kutoka Congo kuanza kuingia magharibi mwa Uganda sasa jitihada zake zote zinalenga kuwafikia maelfu ya watu waliotabakaa milimani eneo la mpaka na kusuluhisha tatizo la msongamo ulio kwenye kituo cha kupitia kilicho umbali wa kilomita 25 ndani mwa Uganda. UNHCR inasema kuwa hadi tarehe 18 mwezi huu wakimbizi 15,500 walikuwa wamehamishwa kutoka mwa eneo lisilo salama hadi kwenye kituo cha Bubukwanga ambapo kuna usalama na huduma zingine. Kituo hicho kinasimamiwa na Shirika la msalaba mwekundu nchini Uganda na kina uwezo wa kuwahifadhi watu 25,000. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN)

UNHCR na washirika wa serikali wanatumia malori 15 bila kusimama siku nzima wakiwahamisha wakimbizi na mali zao kwenda kituo hicho. Tumehamisha wakimbizi kutoka shule zote za msingi ambapo wamekuwa wakiishi. Eneo ambapo wakimbizi 5000 wamesalia ni shle ya msingi ya Butogo

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter