FAO yawapiga jeki wakulima wadogo wadogo Lebanon

19 Julai 2013

Kwa miaka mingi Lebanon imekuwa ikiagiza chakula toka nje kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya watu wake lakini kutokana na mpango huo wa FAO huenda hali hiyo ikapungua.

Sekta ya kilimo inatajwa kuwa ndiyo uti wa mgongo wa taifa hilo ambalo wananchi wake wengi wanategemea kujiingizia kipato.

Utafiti mmoja ulioendeshwa na FAO hivi karibuni katika maeneo ya Akkar, Baalbek, Hermel, Beqaa, na Rashaya ulibaini kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wakulima ni maskini.

Kutokana na hali hiyo FAO imeanzisha juhudi za kuwakwamua wakulima hao hatua ambayo inaelezwa kuwa inaweza kusaidia kukuza ajira.