Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yabaini hatari za kiafya zinazokabili makundi ya wahamiaji wanaoelekea Kusini mwa Afrika

IOM yabaini hatari za kiafya zinazokabili makundi ya wahamiaji wanaoelekea Kusini mwa Afrika

Matokeo ya awali ya utafiti mpya uliofanywa na shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM kwa ubia na taasisi ya masuala ya afya Kusini na mashariki mwa Afrika, PHAMESA) yanaonyesha hatari za kiafya zinazowakabili raia wanaohama makwao kutoka nchi za Maziwa makuu, Afrika Mashariki na hata pembe ya Afrika kuelekea Kusini mwa Afrika. Matokeo hayo yamewasilishwa kwenye mkutano wa pili wa mawaziri wa nchi za kusini mwa Afrika kuhusu mashauriano juu ya uhamiaji huko Maputo, Msumbiji. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM na anaelezea kile hasa kilichobainika.

(SAUTI YA JUMBE)