Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rasimu ya sheria ya vyombo vya habari Somalia iangaliwe upya: UM

Rasimu ya sheria ya vyombo vya habari Somalia iangaliwe upya: UM

Ofisi ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu imetaka kupitiwa upya kwa rasimu inayohusu sheria ya vyombo vya habari nchini Somalia.

 George Njogopa na maelezo Zaidi:

 (Taarifa ya George) 

Ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imeitaka mamlaka ya Somalia kuangalia upya rasimu hiyo ili iweze kwenda sawia na viwango vya haki za binadamu. 

Imesema kuwa rasimu hiyo iliyopitishwa na baraza la mawaziri inamapungufu makubwa ikiwemo kutoweka bayana kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.

Rasimu hiyo inawataka waandishi wa habari kutaja vyanzo vyao vya habari na inawabana kutoaandika taarifa zinazokwenda kinyume na misingi ya uislamu na utamaduni wa Somalia. 

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT)