Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani imeimarika Côte d’Ivoire, sheria zitekelezwe: UM

Amani imeimarika Côte d’Ivoire, sheria zitekelezwe: UM

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali ya amani nchiniCôte d’Ivoire aambapo wajumbe wa baraza hilowameelezwa kwamba licha ya hatua kubwa ya usalama iliyopigwa na taifa hilo ambalo lilikumbwa na mzozo baada ya uchaguzi mkuu, hatua zaidi za utekelezaji wa haki za binadamu zinahitajika

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kikao hicho mjini New York Msaidizi wa KatibuMkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu operesheani za amani Herve Ladsous amesema ni muhimu Côte d’Ivoire kutafuta namna ya kuzuia migogoro katika ngazi ya kijamii na kukuza upatanisho utakao kwenda sambamba na haki na sheria.

Akiongea kupitia mtasfiri huyu anasema

"Upatanisho lazima uende sambamba na usawa na haki, kuhakikisha uwajibishwaji wa uvunjaji wa haki za binadamu na haki za kimtaifa za binadamu ni nguzo , haki za binadamu zinabaki kuwa muhimu na hapa najumuisha matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na kingono, juhudi za kutokomeza uvunjaji wa sheria lazima zitekelezwe kwa kuhakikisha kwamba wale waliovunja sheria wanafikishwa katika vyombo vya sheria bila ya kujali nafasi zao za kisiasa."

Hata hivyo amesema mafanikio makubwa ya kumarika kwa amani nchini humo ni ishara tosha ya kazi iliyofanywana Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Côte d’Ivoire UNOCI, ambao uliongezwa muda wake hadi July 31 2013.