UM kusaidia kutokomeza kipindupindu Haiti

18 Julai 2013

Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos ametangaza mgao wa ziada wa dola za Marekani1.5 kutoka Mfuko wa Dharura (Cerf) ili kukabiliana na kipindupindu nchini Haiti. fedha za nyongeza ziinakuja wakati muhimu, ambapo wagonjwa wa kipindupindu wanatarajiwa kuongezeka kwa ajili ya msimu wa mvua.

Ugonjwa huu umepelekea watu 8100 kupoteza maisha yao na zaidi ya watu 660,000 wameambukizwa tangu mlipuko wa kipindupindu Haiti mwaka 21010 amesema Mratibu wa maswala ya kibinadamu OCHA, John Ging na kuongeza kuwa ni muhimu kuzuia vifo zaidi vitokanavyo na ugonjwa huo.

Fedha hizo zitasaidia washirika wa kibinadamu kutoa tiba katika maeneo ya hatari, Mgao huu umeleta jumla ya fedha kwa ajili ya dharura kukabiliana na kipindupindu nchini Haiti mwaka huu kufikia dola milioni 4. Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa pia hivi karibuni ulitangaza zaidi ya dola milioni 1 kwa ajili ya kukabiliana na kipindupindu. Hata hivyo, fedha zaidi zinahitajika haraka. Kando ya dola 34.5 ambazo mashirika ya kibinadamu yalikuwa yameomba kwa mfuko wa kukabiliana na kipindupindu mwaka 2013, dola milioni 5.7 tu zimepatikana hadi sasa.

Ukosefu wa fedha umeathiri uwezo wa kukabiliana na kipindupindu nchini Haiti. Huku idadi ya mashirika ya kibinadamu ya kushiriki katika kukabiliana ikishuka hadi chini ya nusu ya ile ilikuwa mwaka 2012, na kuna pengo kubwa katika chanjo katika kaskazini ambapo kesi nyingi mpya zimerekodiwa.

Umoja wa Mataifa unafanya kazi na Serikali ya Haiti na asasi za kiraia kuimarisha uwezo wa kitaifa, sambamba na mpango wa Katibu Mkuu wa kusaidia Mpango wa Taifa wa Kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu, pamoja na kukabiliana na mlipuko wa sasa.