Watoto wakumbwa na madhila ya vita: UM

Watoto wakumbwa na madhila ya vita: UM

Mwakilshi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na athari za kivita Leila Zerrougui amekamilisha ziara yake nchini Syria , Jordan, Iraq, Turkey, na Lebanon ambako ameshuhudia madhara ya mgogoro wa Syria kwa watoto waliko nchini humo na katika ukanda huo kwa ujumla.

Akitoa tathimini ya ziara hiyo Bi Zerrougu amesema amekutana na wazazi ambao watoto wao walikufa kwa milipuko ya bomu, watoto ambaoa kaka au dada zao waliuwauwa mbele ya machoyaona watoto waliojeruhiwa vibaya na hawakutarajiwa kama wangeishi tena.Pia amekutana na maafisa wa serikali , wawakilishi wa vikundi vya upinzani na kuwataka kuchukua hatua za dharura katika kuwalinda watoto na raia.

 Bi Zerrougu amesema watu milioni sita na laki nane wanahitaji msaada wa dharura nusu yao wakiwa ni watoto. Pia ameitaka serikali ya Syria amabayo hivi karibuni imepitisha sheria ya kupinga ajira kwa watoto kuitekeleza huku akionya juu ya taarifa ya watoto kuwekwa kizuizini.

Mwakilishi huyo maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na athari za kivita amesema watoto nchini Syria hawajenda shule kwa miezi kadhaa jambo linalo hatarisha kizazi kijacho kuwa kisichojua kusoama wala kuandika .

Kadhalika analifahamisha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa juu ya uuwaji au kulemazwa, ajira, utekwaji , ukatili wa kijinsia mashambulizi katika maeneo ya shule na kukataliwa kwa misaada ya kibinadamu kama mambo ambayo yamechukua nafasi na kuathiri watoto nchini Syria.